Urusi imeendelea na tabia yake ya kufanya udukuzi wa nyaraka za siri za mataifa mabalimbali barani Ulaya na Amerika ambapo kwa kipindi hiki imefanya udukuzi wa nyaraka za siri za Rais wa Ukraine, Petro Poroshenko.
Katika taarifa iliyotolewa na utawala wa Rais huyo imesema kuwa kwa sasa hali imeshadhibitiwa na hakuna tishio lolote katika tovuti ya rais ambayo imekuwa ikitunza nyaraka mbalimbali za siri za Serikali hiyo.
Aidha, kufuatia udukuzi huo uliofanywa na Urusi, Serikali ya Ukraine imepiga marufuku matumizi yote ya mitandao ya Urusi nchini humo huku ikiiwekea vikwazo nchi hiyo kwa kuvunja sheria ya mitandao huku ikituhumiwa kuhusika na mzozo wa masahiriki mwa nchi hiyo.
Hata hivyo, hatua ya kupiga marufuku huduma za mitandao hiyo ya kijamii ya Urusi nchini Ukraine iliyopendekezwa na baraza la usalama la nchi hiyo huenda ikawaathiri raia wengi ambao ndio watumiaji wakubwa.