Baada ya Urusi kusema imekamilisha awamu ya kwanza ya operesheni yake ya kijeshi nchini Ukraine, taarifa zinasema Moscow imeanza kupunguza wanajeshi wake karibu na mji mkuu wa Ukraine, Kyiv.

Marekani na Uingereza zilinukuliwa jana kukili kuona baadhi ya vikosi vya Urusi vikiondoka Kyiv hata hivyo Marekani inaamini ni njia ya Urusi kubadili mkakati wa operesheni yake nchini Ukraine.

Wizara ya Ulinzi ya Urusi ilitangaza kuwa “itapunguza kwa kiasi kikubwa operesheni yake ya kijeshi nje ya Kyiv na Chernihiv, wakati majadiliano ya amani yakiendelea huko Istanbul, Uturuki.

Kwa muibu wa CNN ulilipoti kuwa Urusi ilikua imeanza kuondoa vikosi vya mbinu maalum (BTGs) katika maeneo yanayozunguka mji mkuu wa Ukraine.

Vilevile, Uingereza ilidai kuona vikosi vya Urusi vikiondoka hata hivyo ilisisitiza inataka kuona vikosi vyote vya Urusi vikiondoka Ukraine ili kufikia makubaliano ya amani, Msemaji wa Boris Johnson alisema.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy amepuuzia mpango wa Urusi kupunguza kwa kiasi kikubwa shughuli zake za kijeshi kaskazini mwa Ukraine, akisema “Waukreni sio wajinga” na kuahidi kuendelea na juhudi za kijeshi za kujihami.

Rais Zelenskiy alizungumza katika hotuba yake ya video mapema Jumatano ambapo alisema kuwa “Watu wa Ukraine tayari wamejifunza katika siku hizi 34 za uvamizi na katika miaka minane iliyopita ya vita huko Donbas kwamba ni matokeo madhubuti tu yanayoweza kuaminiwa.”

COSOTA yateta na wahariri

Thiago Silva awapigania Azpilicueta, Christensen, Antonio Rudige
Bumbuli: Tumeialika Mafunzo FC kwa sababu maalum