Rubani mmoja wa ndege shirika la ndege la Myanmar ambae pia ni raia wa Myanmar alilazimika kutua bila gurudumu la mbele baada ya ndege kupata hitilafu ya kiufundi wakati wa kutua.
Kwa mijibu wa BBC ndege hiyo iliteleza kwa muda kwenye barabara ya ndege kabla ya kusimama katika uwanja wa ndege wa Mandalay.
Rubani wa ndege hiyo aina ya Embraer 190 alisifiwa baada ya kutua salama na abiria wote 89 bila ya kuwa na majeruhi.
Ndege hiyo ilikua imepangia kutua katika uwanja wa ndege wa Mandalay ikiwa inatoka Yangon lakini rubani alipojaribu kutua alishidwa kufanya hivyo kutokana na sababu za kiufundi.
Hata hivyo Rubani huyo alifuata taratibu zote za kiusalama ikiwa pamoja na kumwaga mafuta ili kupunguza uzani wa ndege huku ikiteleza katika barabara ya ndege kwa sekunde 25.
“Rubani amefanya kazi kubwa sana,” Win Khant, Waziri wa uchukuzi wa Myanmar, aliliambia shirika la habari la Reuters.
Hata hivyo kisa hichi ni cha pili kutokea Myanmar wiki hii, huku Siku ya Jumatano, ndege ya shirika la ndege la Bangladesh iliteleza na kutoka katika barabara ya ndege ilipotua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Yangon na kuwajeruhiwatu 17.