Teknolojia ya uchukuzi inazidi kuboreshwa siku hadi siku hususani katika nchi zilizoendelea, kwa upande wa usafiri wa nchi kavu huduma ya Taxi ipo ulimwenguni kote lakini kwa upande wa usafiri wa anga huduma hiyo bado ni ngeni kwa watumiaji wa anga, usafiri ambao ni waharaka zaidi.
Nchini Australia huduma ya Taxi za angani inatarajiwa kuanza katika kipindi cha kuanzia miaka mitano ijayo, ambapo tayari mradi wa kisasa wa kiteknolojia wa kusafirisha abiria angani umekwisha anza.
Mamlaka ya safari za anga nchini Australia ijulikanayo kama (CASA), imetoa taarifa kwa wananchi wake kuwa, mradi wake wa kisasa wa kiteknolojia wa kusafirisha abiria angani unakaribia kukamilika.
-
Makala: Wateule watano wa JPM ‘waliokiki’ zaidi 2018 na mambo yao
-
Mayweather atangaza habari itakayomsikitisha Pacquiao
CASA imebainisha kampuni ambayo inasimamia mradi huo imeahidi kukamilisha huduma ya Taxi za angani kwa muda usiozidi miaka mitano kuanzia sasa, ambapo vyombo vya habari nchini Australia vimeripoti kuwa shirika hilo litakuwa likitoa huduma hiyo ya taxi za anga kwa bei nafuu mara tu mradi huo utakapokamilika.
Aidha msemaji wa mamlaka ya anga nchi Australia(CASA ), Peter Gibson amathibitisha kwa kusisitiza kuwa mradi huo unatarajiwa kukamilika ndani ya muda wa mika mitano ijayo kwa asilimia 100.