Bingwa wa mbio fupi duniani, Usain Bolt amejiondoa kwenye michuano ya Paris na ‘Lausanne Diamond League’ kufuatia majeraha yanayomkabili kwa sasa.

Bolt amechukua maamuzi hayo kufuatia maumivu ya mguu ambayo anaamini hayatoweza kumpa nafasi ya kuwa sehemu ya washiriki wa michuano hiyo ambayo imepangwa kufanyika juma hili pamoja na juma lijalo.
Mwanariadha huyo amewaomba radhi mashabiki wake kwa uamuzi huo aliouchukua huku akisisitiza kuwa halikua kusudio lake kufanya hivyo isipokuwa majeraha yanayomkabili.

Hata hivyo, mwanariadha huyo kutoka nchini Jamaica amesema kukwaa kwake pembeni muda huu, kutampa nafasi nzuri ya kujiandaa vilivyo atakapopona majeraha ya mguu, kwa ajili ya michuano ya dunia itakayofanyika mjini Beijing, China mwezi Agosti.

Michuano ya Paris imepangwa kuunguruma siku ya jumamosi ili hali michuano ya Lausanne itashuhudiwa ikiwapambanisha washiriki kutoka kona zote za dunia siku ya Al-khamis ya juma lijalo.

Bolt, mwenye umri wa miaka 28, aliendelea kujikusanyia mashabiki wengi duniani kufuatia umahiri wake wa kufukuza upepo kwa mita 100 kwa kutumia muda wa sekunde na 10.12 pamoja na mita 200 kwa muda wa sekunde 20.13.

Makamba: Anayemwaga Fedha Kusaka Urais Hafai
Blatter Ahofia Kwenda Kutazama Fainali za Wanawake kisa kashfa