Uongozi wa Ihefu FC umewatuliza mashabiki wa klabu hiyo kuhusu mpango wa kuachwa na kusajiliwa kwa wachezaji wapya klabuni hapo, kwa ajili ya msimu ujao 2023/24.

Ihefu FC ni sehemu ya Klabu za Ligi Kuu Tanzania Bara zilizokaa kimya katika kipindi hiki, ambacho Klabu kadhaa zimekuwa zikiendelea kuanika majina ya wachezaji wanaoachwa.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino wa Ihefu FC Peter Andrew amesema, Mashabiki wao wanapaswa kuwa watulivu na wakati wowote Uongozi utakapotoa ruhusa ya kutangazwa kwa Wachezaji wanaoochwa klabuni hapo, watajulishwa kupitia vyanzo vya habari vya klabu hiyo ya mkoani Mbeya.

Andrew amesema Uongozi wao kwa sasa unaendelea na vikao vya ndani sambamba na kupitia ripoti ya Benchi la Ufundi, ambayo inatoa muongozo wa kuachwa kwa Wachezaji na wale watakaosajiliwa kwa ajili ya msimu ujao 2023/24 wa Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’.

“Bado hakuna chochote, tukiwa tayari tutatoa taarifa rasmi katika kurasa zetu.”

“Taarifa zote zinazohusu timu zikiwa tayari tutangaza ila kwa sasa bado hatuna jipya la kuwatangazia umma”.

“Uongozi wetu unaendelea na vikao vya ndani kwa ajili ya kupitia ripoti ya Benchi la Ufundi, nina uhakika kwa asilimia 100 ripoti itatoa muongozo wote wa wanaoachwa na watakaosajiliwa, kwa hiyo tusubiri kila kitu kitawekwa wazi.” Amesema Pater Andrew

Ihefu FC itakatoshiriki kwa msimu wa pili mfululizo wa Ligi Kuu Tanzania Bara tangu ilipopanda msimu uliopita, ambapo ilimaliza ikiwa na alama 39 zilizoiweka kwenye nafasi ya sita katika msimamo wa ligi hiyo.

African Doctors watambia weledi kiuwezeshaji
Maswali tata mabaki mwili wa binadamu Morogoro