Mabosi wa Manchester United wamepanga kuandaa bajeti kwa ajili ya kumsajili kiungo wa Fulham, Joao Palhinha katika dirisha lijalo ikiwa ni siku chache tangu dili lake kujiunga na Bayern Munich lilipokwama katika dirisha lililopita.

Kwa muda mrefu Fuham iliweka wazi inahitaji zaidi ya Pauni 90 milioni ikiwa kuna timu itamhitaji mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil.

Licha ya kusajili viungo kadhaa dirisha lililopita wakiwemo Sofyan Amrabat na Mason Mount, Man United bado inaonekana kuwa na upungufu kwenye eneo hilo.

Faili la nyota huyu limetua kwa kocha wa Man united, Erik Ten Hag, lakini kiasi cha pesa inachotaka Fulham ili kumuuza ndicho kinachotia shaka uwezekano wa dili hilo kukamilika.

Kiasi cha Pauni 90 milioni au zaidi kinaonekana kuvuka bajeti ya Mashetani Wekundu ambao dirisha lililopita ilibidi wapunguze kwanza wachezaji ili kupata pesa nyingine ya kusajili kutokana na kukwepa rungu la UEFA la matumizi makubwa ya fedha.

IGP, Vyombo vya Sheria tazameni na huku
Ally Kamwe: Gamondi anajuwa tunachokitaka