Kiungo wa zamani wa AS Roma, Gaetano Dagostino amesema Romelu Lukaku ataongeza nguvu katika kikosi hicho baada ya kukamilisha uhamisho wa kujiunga na klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya Italia.
AS Roma ilimchukua Lukaku kwa mkopo wa msimu mzima na watalipa ada ya Pauni 8 milioni baada ya kukubaliana na Chelsea, ingawa kiungo huyo hana matumaini kama Lukaku ataisaidia Roma katika mbio za kuwania ubingwa wa Serie A msimu huu.
Dagostino alisema alisema: “Ujio wake utaongeza nguvu katika kikosi, lakini ubingwa sidhani kwa sababu katika idara nyingine bado hazijakamilika, safu ya ulinzi haina nguvu, (kocha) Jose Mourinho anaweza kubadilisha mfumo kutokana na aina ya mawinga waliopo maana hawana ubora wa kucheza mfumo wa 35-2 na 24-2-1.”
Kwa kitendo cha Lukaku kuondoka kwenye timu Chelsea itakuwa imeokoa Pauni 16 milioni kwenye bili ya mishahara yake, lakini hakuna kipengele kinachowalazimisha Mshahara wa Lukaku huko Roma kwa msimu.
AS Roma kumchukua jumla wakati mkopo wake utakapokwisha. Lukaku amekuwa akiwekwa kando kwenye kikosi cha uliopita. Amekiwa akufanya mazoezi na timu ya vijana chini ya umri wa miaka 21.
Kocha mpya wa Chelsea, Mauricio Pochettino ameripotiwa kupiga marufuku kumtumia mshambuliaji huyo wakati anatua, ambaye alinaswa kwa Pauni 97.5 milioni miaka miwili iliyopita akitokea Inter Milan na alifunga mabao 15 katika msimu wake wa kwanza.