Shirikisho la Soka Tanzania ‘TFF’ limethibitisha kuwa Klabu ya Young Africans hadi sasa haijafanya usajili wa Michuano ya Kimataifa (Ligi ya Mabingwa Barani Afrika) msimu ujao 2023/24, hadi sasa.

Mapema leo Alhamis (Julai 20) TFF imetoa taarifa hiyo kupitia vyanzo vyake vya habari, huku Klabu nyingine zitakazoshiriki Kimataifa msimu ujao zikifanya usajili ambao umeshatambuliwa na CAF.

Taarifa hiyo inaonesha hadi sasa Azam FC, Singida Fountain Gate na Simba SC ndizo zimefanya usajili wa Kimataifa ambao unatambuliwa na CAF kupitia TFF.

Hata hivyo hadi sasa haijafahamika kwanini Young Africans haijawasilisha CAF majina ya wachezaji iliowasajili, licha ya kuonekana wakiendelea kuwatambulisha wachezaji ambao wamesajiliwa katika kipindi hiki.

Ikumbukwe kuwa Young Africans ambayo ni Bingwa wa Tanzania Bara itashiriki Ligi ya Mabingwa Barani Afrika sambamba na Simba SC, huku Azam FC na Singida Fountain Gate zikitarajia kushiriki Kombe la Shirikisho Barani Afrika msimu ujao 2023/24.

Chelsea yamng'ang'ania Moises Caicedo
Tanzania inapambana na vita ya uchumi - Chongolo