Baba mzazi wa msanii Diamond Platinumz, Mzee Abdul ameibuka na kuingilia kati malumbano kati ya wanawake wawili Zarinah Hassan na mwanamitindo Hamissa Mobeto waliozaa na mwanae Diamond Platinumz, akiwasihi waaache kurushiana vijembe mtandaoni kwani hakuna mke halali wa kijana wake.

Hivi karibuni kumetokea gumzo mtandaoni kati ya Zarinah na Hamissa Mobeto wakirushiana maneno ya kejeli na dharau ambayo kwa namna moja au nyingine ni maneno ya kubomoa.

Mzee Abdul ameamua kuingilia kati swala hilo nakutoa busara zake.

“Maneno wanayotoleana mitandaoni ni mabaya na yananichukiza mno’’ amesema Mzee Abdul.

‘’Ninawasihi hawa wanawake waache malumbano katika mitandao ya kijamii, kwa sababu kila mmoja amezaa hivyo wote wana nafasi na haki sawa kwa vile hakuna aliyeolewa hadi sasa’’ ameeleza bab Diamond.

Aidha amesema kuwa mwanaye bado hajaoa na huenda mmoja wao akaolewa lakini mwingine akapewa heshima yake kama mzazi,

Amesisitiza kuwa kua uwezekano mkubwa kwa wote wawili kuolewa kwani dini ya mwanae inamruhusu.

Mzee Abdul amemalizakwa kusema kuwa ana uhakika kuwa kila mmoja Kitu mmoja kwa kitendo cha kuzaa na mwanaye, ataambulia chochote kitu kwani wana haki.

 

 

 

 

 

Benki kuu ya Tanzania yazifutia leseni benki tano
Kanisa Katoliki limelaani kuzuiliwa kwa maandamano