Ushindi wa bondia Floyd Mayweather dhidi ya Andre Berto umeonekana kumboa bondia mfilipino, Many Pacquiao anaedaiwa kuwa mpinzani hatari zaidi wa bingwa huyo ambaye hajawahi kupigwa.

Wakati pambano la Mayweather na Berto likimalizika jana na Maywether kutangazwa mshindi, Pacquiao alipost Instagram kipande cha video kinachomuonesha akiwa anachezea piano chumbani na kuandika, “hivi ndivyo ninvyofanya nikiwa ‘bored’ (nimechoshwa kwa tafsiri isiyo rasmi).”

What I do when I’m bored. Hehe

A video posted by Manny Pacquiao (@mannypacquiao) on

Pacquiao ambaye alishindwa na Mayweather katika pambano ambalo lilipewa jina la ‘pambano la karne’ huku ushindi huo ukileta utata na mvutano wa uhalali wake, aliibuka hivi karibuni na kudai kutaka marudiano na bondi hiyo Mmarekani baada ya kubainika kuwa alipewa drip za maji ya kuongeza nguvu kabla hajapanda ulingoni kupambana naye.

Pacquiao alimtaka Mayweather kutostaafu hadi pale watakapomaliza ubishi kwa pambano la marudiano, hoja ambayo haijapenya hata kidogo kwenye masikio ya Maywether anaekiri kuwa bondia huyo mfilipino ndiye aliyewahi kuleta upinzani mkali zaidi kwake.

Ibe Aimwaga Rasmi Nigeria
Diamond Amshawishi Nay Wa Mitego Kuhamia CCM , Nay Amkazia