Ushindi wa ubunge wa jimbo la Singida Mashariki alioupata Tundu Lissu kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) hauna doa baada ya kubarikiwa na mahakama.

Mahakama Kuu kanda Maalum ya Dodoma jana imefuta pingamizi la ushindi wa Lissu lililowekwa mahakamani hapo na aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo hilo kupitia CCM, Jonathan Njau.

Jaji Berkel Sehel aliamua kufuta kesi hiyo baada ya mlalamikaji Njau kuiomba mahakama kuiondoa kesi hiyo akieleza kuwa hataki kuendelea nayo.

Katika kesi ya msingi, Njau alikuwa akipinga matokeo ya uchaguzi uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu na kumpa ushindi Lissu. Aliitaka mahakama kufuta matokeo hayo na kuamuru kura zihesabiwe upya.

Magufuli awanyooshea kidole wakuu wa shule za msingi, sekondari
Magaidi walipua bomu ufukweni