Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, David Silinde amezisihi nchi wanachama wa Taasisi ya Uvuvi ya Ziwa Victoria ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuungana na mamlaka zinazoshughulikia viwanda na biashara na takwimu kuhakikisha mchango wa sekta ya uvuvi unaonekana wazi kwenye pato la Taifa la kila nchi.

Silinde ametoa wito huo jijini Kampala, Uganda alipofungua Mkutano wa Tano wa Baraza la Mawaziri la Sekta ya Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji wa Taasisi ya Uvuvi ya Ziwa Victoria (LVFO) ya Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika tarehe 20 Aprili,2023 jijini humo.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, David Silinde (wa pili kushoto ) akiwa na Mawaziri kutoka nchi za Uganda, Kenya na Burundi baada ya kumalizika kwa Mkutano wa TANO wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la nchi wanachama wa Taasisi ya Uvuvi ya Ziwa Victoria (LVFO) ya Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Kampala.

Amesema, suala la mchango wa sekta ndogo ya uvuvi kuonekana mdogo unatokana na ukweli kwamba mazao ya uvuvi yanahesabiwa katika sekta za kilimo na uzalishaji na mazao mengine yakiingizwa katika mnyororo wa thamani wa sekta nyingine.

Akizungumzia ulinzi wa rasilimali za uvuvi katika Ziwa Victoria Mhe. Silinde amesema uvuvi haramu na uvuvi uliopitiliza unahatarisha uwepo endelevu wa rasilimali za uvuvi na mazalia yake katika Ziwa Victoria na hivyo suala la ulinzi wake lazima litiliwe mkazo.

Simba SC, Young Africans zafutiwa Blue Tick
Usiyoyajua kuhusu mapigano ya Majenerali wawili wa Sudan