Wananchi wa Mtaa wa Mapelele katika Kata ya Ilemi Jijini Mbeya wametakiwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya katika kuzuia na kutokomeza uhalifu, kwani ushirikiano ni silaha kuu ya kuzuia matilio ya kiuhalifu maeneo yote nchini.

Haya yamesemwa na Mkaguzi Msaidizi wa Polisi katika kata ya Ilemi, Elibariki Mambuye wakati akishiriki shughuli mbalimbali wakati wa mazishi ya Bi. Esther Joram Kayange wa Mtaa wa Mapelele katika Kata ya Ilemi.

Amesema, wananchi wa Mtaa wa Mapelele wanatakiwa kuacha kufumbia macho vitendo vya uhalifu na kusisitiza kutoa taarifa mapema kwa Jeshi la Polisi, ili kuchukua hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kuwakamata watuhumiwa wa uhalifu.

Aidha, Mkaguzi Mambuye poa amewataka wananchi wa Mtaa wa Mapelele kudumisha kwa vitendo dhana ya ulinzi jirani kwani itasaidia kuzuia na kutokomeza uhalifu katika mitaa, hasa nyakati za mchana ambapo watu wanakuwa kazini na katika shughuli mbalimbali za maendeleo.

Mapinduzi Gabon: Kiongozi wa mpito achaguliwa
CCM yatoa agizo Wahudumu wa kike Zahanati