Katika hali ya kushangaza, Meya wa mji wa Kusini mwa Mexico – San Pedro Huamelula, Victor Hugo Sosa amefunga ndoa na mamba wa kike anayeitwa Alicia Adriana katika sherehe zilizohususishwa na mambo ya kishirikina na mila za zamani.
Katika tukio hilo ndoa, limeleta tafsiri kuwa ni mfano wa mila ya kuzaliwa ambayo imekuwa ikitekelezwazaidi miaka 230 iliyopita ya utamaduni huo, ambao unaaminika kuleta mavuno mazuri na amani ya vikundi vya Wenyeji wa Chontal na Huave nchini humo.
“Ninakubali kuwajibika kwa sababu tunapendana. Hilo ndilo lililo muhimu. Huwezi kuwa na ndoa bila upendo. Ninakubali kuoana na binti huyu Mamba wa kifalme,” alisema Sosa wakati wa ibada hiyo alipokuwa akila kiapo.
Meya wa mji huyo, anawakilisha mfalme wa Chontal na kuoa binti wa kifalme wa kikundi cha asilia cha Huave ambaye sasa anawakilishwa kama mamba wa kike ukuwa ni muungano wa tamaduni mbili za Wahuave na Wachontales.
Aidha, inaarifiwa kuwa tamaduni hiyo ya harusi huruhusu viunga viwili kuungana na ardhi na kutafuta baraka kwa mvua, kuota kwa mazao, amani na maelewano. na harusi hiyo huruhusu pande zote kuunganishwa na nembo ya Mama Dunia, ikimwomba mwenye nguvu zote kwa ajili ya mvua, kuota kwa mbegu, amani na upatano.
Kumekuwa na hadithi nyingi za kushangaza za wanadamu kuoa wanyama wao vipenzi ili kuzuia ushirikina au kukidhi mapokeo ya zamani, huku ripoti zikionesha kuwa mbwa ndio wanaopendwa zaidi linapokuja suala la ndoa ya binadamu na wanyama, haswa nchini India.