Shirika la Afya Duniani – WHO, limependekeza kuongezwa kwa ushuru wa bidhaa za Pombe na Vinywaji vyenye Sukari, ili kupunguza kwa kiasi kikubwa cha idadi ya watu wanaofariki kutokana na unywaji pombe na ulaji usiofaa.

Mapendekezo hayo ya WHO, yanakuja baada ya kufanya tafiti za viwango vya ushuru, ikisema kwamba kiwango cha wastani cha ushuru kimataifa kwa bidhaa zisizo bora kiafya kilikuwa cha chini, huku ikidai kuwa bidhaa kama vile Mvinyo zimekuwa hazitozwi ushuru katika baadhi ya nchi za Ulaya.

Hata hivyo, kupitia taarifa hiyo WHO inadai kuwa watu milioni 2.6 hufariki kila mwaka kutokana na kunywa Pombe, huku watu milioni 8 wakifariki pia kwa mwaka kutokana na ulaji usiofaa.

Shirika hilo, limesema kuongeza ushuru kutasaidia kupunguza matumizi ya bidhaa hizo na kutoa motisha kwa makampuni kutengeneza bidhaa zenye ubora kwa afya ya binaadamu.

Majeruhi wa mafuriko watibiwa bila kupewa rufaa
Marekani waunga mkono mradi kutokomeza ukeketaji