Mkuu wa Kikosi cha Wapiganaji Mamluki wa Russia, Yevgeny Prigozhin ambaye aliuawa katika ajali ya ndege wiki iliyopita (Agosti 23, 2023), amezikwa faragha kwenye makaburi yaliyoko nje kidogo ya mji alipokulia wa St Petersburg.
Msemaji wa Ikulu ya Urusi ya Kremlin, Dmitry Peskov alisema Rais Vladmir Putin hakutazamiwa kuwepo katika mazihsi hayo, huku akikanusha uvumi kwamba ajali hiyo ilipangwa kama kulipiza kisasi kwa maandamano ya Wagner, yaliyofanyika Juni mjini Moscow.
Aidha, Chombo kimoja cha Habari jijini Moscow kilichapisha taarifa katika mtandao wake wa Telegram kikieleza kuwa, “Kuagwa kwa Yevgeny Prigozhin kulifanyika kwa faragha. Wale wanaotaka kumuaga wanaweza kutembelea makaburi ya Porokhovskoye.”
Katika mazishi hayo, usiri ulikuwa umezingira mipango yote na awali na katika ajali hiyo pia Watu wengine wawili Wakuu wa kundi hilo la Wagner, Walinzi wanne wa Prigozhin na Wafanyakazi watatu pia waliuawa wakati ndege binafsi ya Kiongozi huyo wa Wagner aina ya Embraer Legacy 600 ilipoanguka kaskazini mwa Moscow.