Rais wa Urusi, Vladimir Putin na Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un wamekutana katika ukumbi wa Vostochny mashariki mwa Urusi na kuvunja sintofahamu iliyokuwa imetawala juu ya wapi Viongozi hao watakutana na wakiwa na lengo gani.

Kim Jong-un na Vladimir Putin watafanya mazungumzo kuhusu mahusiano ya kibiashara na mambo ya kimataifa, katika kituo cha kurushia vyombo vya anga ambacho kinadaiwa kutumiwa na Urusi kutengeneza silaha za laser ultra-sonic na radio-frequency.

Rais wa Urusi, Vladimir Putin akimkaribisha Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un. Picha ya Sputnik/ Reuters.

Hata hivyo, mkutano huo kulikuwa na usiri mkubwa wa mkutano huo ambapo Moscow na Pyongyang zilithibitisha ziara yake ya Urusi pekee, bila kutaja ni wapi anaelekea au mazungumzo yao yatafanyika eneo lipi.

Wakati kiongozi maarufu duniani anapokwenda nje ya nchi, ziara hiyo hutangazwa mapema na Waandishi wa habari hufahamishwa,
Lakini hilo haliokuonekana wakati wa ziara za Kim Jong Un.

Wadau washauriwa kunadi Utalii, mazao ya Nyuki kibiashara
Wanawake gombeeni nafasi za Uongozi - UN WOMEN