Mwanamuziki mahiri wa hip hop kutoka nchini marekani Cardi B amewashauri mashabiki wake kuipa kipaumbele ndoto ya kutengeneza pesa zaidi na sio kutamani kuwa maarufu huku akiweka wazi kuwa umaarufu ni ugonjwa unaomsumbua sana kwa sasa.
Card b amejaribu kuweka bayana kiwango cha kuchoshwa kwake na umaarufu mkubwa alionao duniani huku akibainisha kuwa licha ya mengi makubwa aliyoyapata kupitia nafasi zilizotengenezwa na umaarufu wake, bado anaamini kuwa ni heri kutokuwa maarufu lakini uwe na uwezo mkubwa wa kifedha.
Card ametilia mkazo kwamba umaarufu wake wakati mwingine humfanya kuwa mgonjwa na hata kujutia umaarufu wake uliotokana na kazi yake ya muziki.
“Wengi wenu mnatamani kuwa maarufu na matajiri, usitamani kuwa maarufu, tamani kuwa tajiri, auhitaji umaarufu. kwa sababu mara tu unapokuwa maarufu huwezi kuwa wewe, huwezi kufanya chochote, unakuwa mfungwa, huwezi kuwa na uhuru wa kufanya mengi ambayo nje ya umaarufu ungeweza kuyafanya.
Ninaumwa na umaarufu, siku zote nimekuwa mfungwa wa umaarufu,, nimechoka kuwa maarufu, sina sauti tena, siwezi kusema chochote” amesema Cardi B.
Aidha rapa huyo ameendelea kusisitiza kuwa anatamani kurejea enzi zile alizokuwa akicheza na kupata pesa bila kujulikana na mtu yeyote duniani kwa kuwa wakati huo alikuwa huru kufanya au kuamua chochote alichojisikia bila ya shaka ya namna yeyote.
Card ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na mashabiki wake kupiti kwenye ukurasa wake maalum wa mtandao wa Instagram (Insta Live) muda mfupi baada ya kutoka kwenye hafla ya Met Gala.
Card B ni miongoni mwa wasanii vinara wakike wenye kufanya vizuri kwenye tasnia ya muziki duniani ambaye alianza kufahamika zaidi mnamo mwaka 2013 kutokana na videos zake kuenea kwa kasi kwenye mitandao mbali mbali ya kijamii hasa wa instagram.
Ingawa umaarufu mkubwa wa nyota huyo ulianza ramsi mwaka 2014, huku thamani yake kwenye kiwanda cha muziki ikichagizwa na wimbo wake bora uliojizolea umaarufu mkubwa ‘Bodak Yellow’ aliouachia rasmi mwaka 2017.
Wimbo uliopata umaarufu mkubwa na hata kuchumpa mpaka nafasi za juu kwenye chati mbali mbali za muziki duniani , na baadae kuchaguliwa kuwania tuzo za Grammy 2017 katika vipengele viwili tofauti ‘Best rap performance na ‘Best rap song’.