Je umesha wahi kuangalia tofauti ya vidole vyako vya mkono wa kushoto, kwa kawaida kwa wanawake kidole cha pili kutoka kidole gumba na kidole cha pete huwa vina urefu sawa.
Wanawake ambao vidole vyao vya pete na kidole kinachofuata baada ya kidole gumba katika mkono wa kushoto vina urefu tofauti wana uwezekano mkubwa wa kuwa na mahusiano ya jinsia moja.
Ripoti hii ni kulingana na utafiti uliofanywa katika chuo cha Essex ambapo wanasayansi walipima jozi 18 za vidole vya mapacha wa kike wanao fanana, ambapo mmoja alikuwa sawa na mwingine ni shoga.
Kwa wastani, wale waliokuwa katika mapenzi ya jinsia moja walikuwa na ripoti tofauti ya ukubwa wa vidole ambapo kawaida ni tabia ya kiume lakini hii ni kwa mkono wa kushoto pekee.
Wanasayansi hao wamebainisha kuwa hali hiyo ni matokeo ya kuwa na homoni za testosterone kwenye tumbo.
Lakini pia Wanasayansi hao walipima dazeni 14 ya vidole vya mapacha wakiume wanao fanana, ambapo mmoja alikuwa sawa na mwingine alikuwa shoga, lakini hawakuona uhusiano wowote.
Wanawake na wanaume walipata homoni za kiume za testesterone wakiwa bado tumboni, lakini baadhi wanaweza kuwa walipata homoni hizo nyingi Zaidi tofauti na wengine, wanasayansi wanasema.
“Kwasababu mapacha wanao fanana ambao wana shea asilimia 100 ya jenes wanatofautiana katika mwelekeo wao kijinsia sababu zingine tofauti na sababu za kijenetiki lazima zinahusika.
Tafiti zinasema kwamba jinsia zetu zinatambuliwa ndani ya tumbo na inategemea kiasi cha homoni za kiume ambazo mtu amezipata akiwa tumboni au namna mwili wa kila mtu unavyo pokea homoni hizo, na wale ambao wanapata homoni hizo za kiume kwa kiwango cha juu wana uwezekano kuwa mashoga au watu wanao weza kuwa na mahusiano na jinsia yoyote ile.
“Kwasababu ya uhusiano kati ya kiasi cha homoni na utofauti katika urefu wa vidole, kuagalia mkono wa mtu kunaweza kukudokeza jinsia zao”.
Matokeo hayo yamechapishwa katika hifadhi ya Tabia za mahusiano ya kingono