Mtaalam wa masuala ya Afya ya Uzazi huko nchini Kenya. Dr. Shaunak Khandwala amesema kwamba wanaume wengi wanaokula ugali kwa wingi wana hatari ya kushindwa kuwazalisha wake zao kutokana na kuzalisha mbegu za Kiume chache na dhaifu.

”Ugali mwingi mwilini una matokeo hasi katika mfumo wa uzazi wa mwanaume kwani unasababisha mwanaume kuwa na uwezo wa kutengeneza mbegu za kiume chache na dhaifu kutokana na mahindi kutoa sumu iitwayo Aflatoxins” .Dr. Shaunak Khandwala.

Wataalamu wanasema sumu hiyo hupunguza uwezo wa mwanaume kutengeneza mbegu za kiume kwa wingi na kumfanya mwanaume ashindwe kutungisha mimba.

Kwa mujibu wa chombo cha habari cha Standard Digital nchini Kenya kimesema kuwa ulaji ugali na maziwa kwa wingi kwa wananchi wa Kenya kutasababisha wanaume washindwe kutungisha mimba.

Na hii ni baada ya utafiti uliofanywa na chuo cha International Livestock Reseach mwaka 2016.

Ambapo chuo hiko kimebainisha hayo mara baada ya kugundua kuwa maziwa na mahindi mengi yanayouzwa nchini Kenya yana miliki kiwango kikubwa cha sumu aina hiyo ya Aflatoxin.

Ambapo asilimia 95 ya aina 403 za mahindi yanayolimwa na kununuliwa na familia nyingi nchini humo yana miliki aina hiyo ya sumu yenye madhara makubwa kwa wanaume.

 

Sokwe mtu wasimama kupiga picha na Askari wanyama pori
Umoja wa Afrika waingilia kati maandamano Sudan

Comments

comments