Hatimaye taasisi ya TWAWEZA imetoa utafiti wake juu ya hali ya siasa nchini zikiwa zimebaki siku 32 kabla ya kupiga kura ya kumchagua rais, wabunge na madiwani.

Kwa mujibu wa tafiti hizo, endapo kura zingepigwa leo, mgombea urais kupitia CCM, Dk John Magufuli angeshinda kwa asilimia 65 dhidi ya mpinzani wake mkuu kupitia Chadema anayeungwa mkono na vyama vya upinzani vinavyounda Ukawa, Edward Lowassa, akipata asilimia 25.

Katika utafiti huo, watu 1848 ndio waliohojiwa.

Twaweza wameeleza kuwa utafiti huo ulifanywa katika maeneo ya mijini na vijijini na kwamba hawakutaja jina la mgombea bali majina yote yalitajwa na wananchi hao. Hata hivyo, utafiti huo umeonesha kuwa wananchi wengi hawafahamu vyama vilivyosimamisha wagombea urais. Kupitia swali lilikuwa kwenye dodoso likimtaka mwananchi kueleza chama ambacho angekichagua katika nafasi ya urais, vyama vya NCCR Mageuzi, NLD, CUF, na Chadema vinaonekana kwenye jedwali la majibu. Hata hivyo vyama hivyo vilipewa alama ya chini zaidi kulinganishwa na CCM iliyobeba asilimia 60.

Kadhalika, matokeo yanayotokana na swali lilikuwa kwenye Dodoso likiwataka wananchi kutaja jina la mgombea urais ambaye ana sifa hizo, ambapo alama za jumla zilionesha mgombea urais kupitia CCM anaongoza.

“Ifahamike kuwa, watu wanaweza kubadilisha maamuzi wakati wowote kuanzia sasa kwa jinsi ambavyo Utafiti unaonyesha,” walisema Twaweza.

Rasmi NI Star Times First Division League
Neymar Amuita Kiaina Philippe Coutinho FC Barcelona