Watafiti wa masuala ya urembo na mwenekano wa sura wametoa matokeo ya utafiti wao kuhusu mwanaume maarufu mwenye macho yenye mvuto zaidi duniani, wakimtaja mwimbaji Harry Styles.

Utafiti huo uliochapishwa na taasisi ya Uingereza inayohusika na masuala ya urembo, vipodozi vya usoni na upasuaji wa kubadili mwili inayojulikana kama ‘Centre for Advanced Facial Cosmetic and Plastic Surgery’ imemtaja mwimbaji huyo ambaye ni mmoja kati ya waasisi wa kundi la One Direction kuwa mshindi huku wakiweka wazi njia waliyotumia kufanya mchujo.

Watafiti hao wamedai kuwa pamoja na mambo mengine, walitumia kipimo cha ‘Golden Ratio’ kinachojulikana kama ‘Phi’. Kipimo hicho ni maalum kwa kuangalia jinsi ambavyo sura ya mhusika ilivyokaa kwa vipimo vya umbali wa macho na pua. Wamedai Harry Style alipata wastani wa asilimia 98.15 ya ukamilifu uliotakiwa.

Mwimbaji huyo amewafunika waliokuwa washindani wake wakubwa katika kipengele hicho ambao ni Will Smith, Brad Pitt, George Clooney na Idris Elba.

Harry pia amefunika katika kipengele cha mwanaume maarufu mwenye pua lenye mvuto zaidi. Waliokuwa washindani wake wakuu kwenye kipengele hicho nii Jamie Foxx, David Beckham, Idris Elba na Ryan Gosling.

Matokeo kuhusu macho yalikuwa kama ifuatavyo:

  1. Harry Styles 98.15%
  2. Will Smith 97.75%
  3. Brad Pitt 97.75%
  4. George Clooney 94.8%
  5. Idris Elba 93.65%

 Our take: Huenda utafiti huu haukulimulika vizuri bara la Afrika ambalo limebarikiwa sio tu kwa maliasili bali pia kwa uzuri asili.

Makamu wa Rais Kenya azungumzia tukio la uvamizi nyumbani kwake
Polepole asema waliojuzulu ndani ya CCM wamesababisha hasara