Ngozi ni kiungo muhimu sana katika mwili wa binadamu. Inafanya kazi mbalimbali kama vile kuulinda mwili, kusaidia kutoa takamwili, kusaidia kuratibu joto, maji na chumvi ya mwili pamoja na kuhisi vichocheo kama vile joto, baridi, miguso na mkandamizo kutoka nje ya mwili.
Richa ya hayo ngozi ni sehemu muhimu sana katika muonekano na uzuri wa mwili. Ngozi ikiwa nzuri na mwili huwa vizuri, ngozi ikiwa vibaya na mwili pia huweza kuwa vibaya.
Ngozi kavu ni aina ya ngozi yenye upungufu wa mafuta na maji ya kutosha kuweza kuifanya iwe na afya njema, kuifunika na kuiunganisha ili iwe katika hali nzuri. Matokeo yake seli za ngozi hunyauka, huachana na hata kuwa kama magamba na kuweza kubanduka. Ikizidi ngozi kavu huanza kupasuka na kuwa na vidonda na maumivu.
Ngozi kavu hutokana na kufeli kwa mfumo wa kuweka sawa kiasi cha maji na mafuta katika ngozi yaani maji na mafuta yanayozalishwa, yanayoingia, yanayotoka na yanayoondolewa.
Hali hiyo husababishwa na Mtu kutokunywa maji ya kutosha, Kuunguzwa na jua na joto kali vinavyofanya maji mengi kupotea, Matumizi ya vipodozi vikali vinavyoharibu ngozi na mfumo wa maisha ya ngozi, Ngozi kuzeeka, Ukosefu wa mlo kamili (bora), Kemikali zinazokausha ngozi kama vile kemikali za kusafishia sabuni za kufulia na kuoshea vyombo na Kemikali za kuua vijidudu zenye asili ya pombe (Kwa mfano Spiriti), Ngozi kutofunikwa na mafuta ya kutosha kuzuia maji yasipotee.
-
Hizi hapa sababu 7 za kutumia chai ya kahawa
-
Makala: Vyakula vitakavyokuza nywele zako haraka na kuzipa afya
Kuna matatizo kadha wa kadha yanayotokana na ngozi kavu, yakiwemo ngozi kuzeeka kwa haraka kuliko kawaida hii ni kutokana na kasi ya kufa kwa seli kuwa kubwa zaidi na afya ya seli zake kuwa dhoofu, Pili ngozi kavu ni rahisi zaidi kupata maambukizi, magonjwa na majeraha. Kadiri ukavu wa ngozi unavyozidi ndivyo magonjwa yanavyokuja na kuiharibu zaidi ngozi, Pia ngozi kavu ni kwamba hunyauka na kusinyaa, na kufanya muonekano wa ngozi usiwe mzuri.
Hivyo endapo utakuwa na tatioz la kuwa na ngozi kavu ni vyema kuchukua hatua mapema ili kuepukana na tatizo hilo.