Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  kupitia chama cha mapinduzi (CCM), Dkt.John Pombe Magufuli amewaahidi wakazi wa Maganzo mkoani Shinyanga kuwa ataishughulikia migogoro ya ardhi baina ya wakazi na wawekezaji katika eneo hilo.

Dkt. Magufuli ameahidi hayo wakati mkutano wake wa kampeni za uchaguzi mkuu, katika jimbo la Kishapi mkoani hapo akiwataka kumuachia jukumu hilo kwakuwa mamlaka yote ya ardhi yapo chini ya usimamizi wa rais.

Magufuli amemtaka mgombea ubunge wa jimbo hilo kupitia CCM, Boniphace Butondo, kuanza na suala hilo iwapo atachaguliwa kuwa mbunge katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, mwaka huu.

“Mimi ni mtumishi wenu, ninaomba hili mniachie, naomba mniachie na mheshimiwa mbunge, utakapoteuliwa, hii ndo ikawe kazi yako ya  kwanza”. amesema Dkt. Magufuli.

Dkt. Magufuli ameeleza hayo akiwa njiani kuelekea mkoani Simiyu, kuomba ridhaa ya wananchi kumpigia kura asalie madarakani kwa muhula wa pili.

JPM: Tutaendelea kutoa elimu bila malipo
Kampuni ya Total yawajibu wanaodai inaondoka Tanzania

Comments

comments