Panaitwa Mwamba wa Riyom, ni mojawapo ya kivutio kizuri sana nchini Nigeria kilicho kando ya barabara ya Jos kuelekea Abuja, Mwamba huu wa Riyom rock upoo katika Mji wa Riyom uliopo kilomita 25 kuelekea kusini-magharibi mwa Jos na 75km kutoka mji mkuu wa Nchi hiyo Abuja.

Ni maarufu zaidi kati ya miamba hiyo ya mawe matatu yanayojulikana kienyeji kama ‘Beta Betat’ ambayo hutafsiriwa kuwa ‘mawe matatu’. Jinsi mawe yamejipanga juu ya kila mmoja ni siri isiyofahamika ya uumbaji na urefu wake ni usawa wa jengo la ghorofa tatu na huwa unawashangaza watazamaji.

Lakini watalii wakaenda mbali zaidi na kuuita mwamba huo Burger rock, wakidai umefanana sana umbile la Burger kutokana na kila moja ya miamba mitatu iliyopangwa kulingana na ukubwa wao juu ya kila mmoja, na katikati ya kwanza, jiwe kubwa hutengeneza umbo zuri ili kusawazisha jiwe la pili.

Hata hivyo, mpangilio wa mwamba huo unapingana na mvuto na ncha yake juu ya mwamba mwingine na mwili mzima juu, ukitazama Riyom kutoka pembe fulani unatoa umbo la jimbo la Plateau kwenye ramani ya Nigeria, kiukweli Dunia ina mambo mengi ya kustaajabisha na ndio maana Wahenga walisema “TEMBEA UONE”.

Habari Kuu kwenye Magazeti ya leo Oktoba 17, 2023
Vijiji 9,671 vimepata huduma ya maji - Aweso