Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania – TANAPA, Dkt. Noelia Muyonga amewataka wazazi na walezi kuwafunza Vijana wao mila na desturi zilizo njema, ili kuendeleza utamaduni wa Mtanzania kwani kitendo hichi kinarithisha utalii.

Dkt. Noelia ametoa kauli hiyo jijini Dodoma wakati akifunga tamasha la Utamaduni la Asili Yetu la Mkoa wa Dodoma ambalo limejumuisha vikundi 27 vya ngoma za asili kutoka wilaya zote za mkuoa huo.

Amesema, “nimefurahishwa nilipoona vikundi vilivyo ‘perform’ leo, mmefanya vizuri sana kuwaleta watoto, watoto walikuwa wanapiga ngoma kwa ufasaha kabisa na kufurahia. Kwa hiyo tuwatie moyo tunapohamasisha watoto kupenda ngoma za asili na maadili yanaendanda na mila na desturi zilizo njema, hatuwezi kutenganisha Utamaduni, Sanaa na Utalii.”

Aidha, Muyonga ameongeza kuwa’ “tuendelee kuhamisha kwa bidi zetu zote utalii huu uhamie kwenye utalii wa kiutamaduni, maana tuna utajiri mkubwa kwenye mikoa yote maana kuna makabila zaidi ya 120 hapa nchini, tukisimama kwa pamoja tukatangaza kila mahali mil ana utamaduni wetu, tutaongeza thamani ya Utalii hapa kwetu Tanzania.

Akimkaribisha Mgeni Rasmi kwenye tamasha hilo, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Dkt. Resani Mnata alisema mchanganyiko wa washiriki wa tamasha hilo ambao unajumuisha Watoto, wanafuinzi wa shule za msingi na sekondari pamoja na wageni wengine umepangwa hivyo kwa lengo la tamasha hilo ni kuiwarithisha Watoto, vijana watu wengine kuujua na kuendeleza urithi wa utamaduni kwa kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

Kwa upande wake Mratibu wa Tamasha la Yamnyausi Organization for Arts and Sports (YOAS), Stewart Mwaluko tamasha hilo linahusisha ngoma za asili kutoka katika Wilaya zote saba za Mkoa wa Dodoma na kupata vikundi vitatu ambavyo ndivyo vilishinda katika Wilaya zao ikiwa ni hatua ya kutangaza vivutio vilivyopo mkoa wa Dodoma.

Ahmed Ally: Nipo tayari kutimuliwa Simba SC
Mila: Wafanya tamasha kumuaga marehemu