Kamati ya Miss Tanzania imetangaza kuzunguka kanda zote nchini kuanza kuwafanyia usaili washiriki wa shindano hilo na kuachana na utaratibu wa zamani wa kutumia mawakala, utaratibu huo mpya wa kutafuta warembo watakao shiriki katika shindano la miss Tanzania unatarajia kuanza machi 2020.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa kamati hiyo Basilisa Mwanukuzi wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Amesema kuwa utaratibu huo utasaidia kuondoa changamoto mbalimbali zilizojitokeza kwa baadhi ya mawakala amabo hawakuwa waaminifu.
Aidha amezitaja changamoto hizo kuwa ni kusimamia warembo, utoaji wa zawadi kujaza na urudishaji fomu kwa wakati iliwarembo waweze kufanyiwa usaili.
”Usaili utaanza kanda ya kati machi 7 , jijini Dododma, Kanda ya kaskazini machi 14, kanda ya ziwa machi 28, kanda ya mashariki april 4, kanda ya vyuo vikuu aprili 21, kanda ya nyanda za juu kusini aprili 11 na kanda ya dar es salaam mei 2, 2020” amesema Mwanukuzi.
Hata hivyo amesema kuwa Miss Tanzania mwaka 2020 itajikita kutangaza misitu na utalii wa asili, uhamasishaji wa kupanda miti katika kila kanda.