Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imegawanya eneo la Jiji katika kanda za kiutawala, ili kurahisisha utoaji wa huduma zenye ubora na usawa kwa jamii kwa kuzingatia utawala bora na kutumia kikamilifu rasilimali zilizopo.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Bi. Tabu Shaibu amesema kuanzishwa kwa huduma za Kanda kutaongeza wigo wa ukusanyaji wa mapato kwa kuwa ufuatiliaji wa walipa kodi utafanyika kwa ukaribu na ufanisi, na kuiwezesha Halmashauri kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

“Kuwepo kwa kanda kutasaidia kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali za wananchi kwa wakati kwa kuwa wakati mwingine matatizo ya wananchi yanashindwa kutatuliwa kwa wakati kwa sababu ya umbali wa kuzifikia huduma wanazozihitaji,” amesema Bi. Shaibu.

Aidha, amezitaja kanda hizo saba za kutolea huduma kuwa ni pamoja na ile namba moja yenye Kata za Kivukoni, Kisutu, Upanga Mashariki na Upanga Magharibi na Ofisi ya Kanda itakuwa katika ofisi ya Kata Upanga Mashariki.

Kanda namba mbili ina Kata za Ilala, Mchikichini, Jangwani, Kariakoo, Gerezani na Mchafukoge, Ofisi ya Kanda itakuwa katika ofisi ya Kata Gerezani na Kanda namba tatu ikihusisha Kata za Buguruni, Mnyamani, Vingunguti, Kipawa, Minazi Mirefu na Kiwalani. Ofisi ya Kanda itakuwa katika Ofisi ya Kata ya Mnyamani na Kanda namba 4 itajumuisha Kata za Tabata, Liwiti, Kimanga, Kisukulu, Segerea, Bonyokwa na Kinyerezi.

Azam FC yafunika kombe Senegal
Simba SC yamsajili mbadala wa Jonas Mkude