Imam mwenye ushawishi mkubwa nchini Mali Mahmoud Dicko ameutaka uongozi wa jeshi nchini humo kukubaliana na madai ya viongozi wa mataifa ya Afrika magharibi kumteua rais raia pamoja na waziri mkuu ifikapo Septemba 15 ili kupunguza vikwazo vilivyowekwa baada ya mapinduzi mwezi uliopita. 

Hatua hiyo imekaribishwa na mataifa 15 wanachama wa jumuiya ya kiuchumi ya mataifa ya Afrika magharibi ECOWAS, lakini vikwazo vimeendelea kuwapo. 

Itakumbukwa siku ya Jumamosi uongozi huo wa kijeshi ulianza mazungumzo na vyama vya kisiasa nchini Mali pamoja na makundi ya asasi za kiraia kuhusiana na hatua za mpito kuelekea utawala wa kiraia.

Dicko, mhubiri wa nadharia za Kisalafi katika dini ya Kiislamu ambaye mapema mwaka huu alichochea maandamano wakati wa maandamano ya kuipinga serikali, aliliambia shirika la utangazaji la taifa hilo jana kuwa Mali inahitaji msaada na kwamba haina itakachopata kwa kwenda kinyume na jumuiya ya kimataifa.

Mwarobaini wa kusaidia wakulima na walaji huu hapa
Kiongozi wa upinzani akamatwa - Belarus