Hali ya utekelezaji wa Sheria za Kazi, Usalama na afya pamoja na hifadhi kwa jamii katika baadhi ya viwanda jijini Dar es Salaam imekuwa si ya kuridhisha, huku Serikali ikitoa siku 14 kwa Kiwanda kimoja cha kuzalisha bidhaa za Plastiki kushughulikia changamoto mbalimbali za Wafanyakazi ndani ya siku 14.

Hayo, yamebainishwa na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Patrobas Katambi mara baada ya kufanya ukaguzi katika Viwanda kadhaa jijini Dar es Salaam kikiwemo kilichopewa agizo hilo cha Buza, Wilayani Temeke.

Naibu Waziri – Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Patrobas Katambi akizungumza na wawekezaji wa kiwanda cha kuzalisha bidhaa mbalimbali za chuma.

Amesema, “kuna ukiukwaji mkubwa wa taratibu za usalama na afya ikiwemo wafanyakazi kutopatiwa vifaa vya kujikinga na vihatarishi vya magonjwa na ajali. Hali ya mazingira ya kazi sio nzuri kuna mzunguko finyu wa hewa na hata mwanga hautoshelezi.”

Aidha, Katambi ameongeza kuwa, “kuna ukiukwaji wa haki nyingine za wafanyakazi ikiwemo ujira mdogo, wafanyakazi kulazimishwa kufanya kazi kwa zaidi ya masaa yanayoruhusiwa kisheria bila kupatiwa malipo ya ziada pamoja na kutowasilisha michango ya wafanyakazi katika mifuko ya hifadhi kwa jamii.”

Man Utd yaweka Milioni 40 kwa Onana
Twaha Kiduku kizichapa na Mbrazil