Rais wa Jarmhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amewateuwa washauri wa Rais – Siasa na Uhusiano wa Jamii wanne, akiwemo Mbunge wa Jimbo la lsmani, William Lukuvi na Mbunge Mstaafu Abdallah Bulembo.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu iliyotolewa kwa vyombo vya Habari, imesema pia Rais Samia amewateuwa aliyewahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji Balozi
Rajab Omar Luhwavi na Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi na Waziri Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar. Haji Omar Kheir.

Mwinyi aishukuru Korea maendeleo uchumi wa buluu
Zanzibar kunufaika na biashara ya Kaboni - Wizara