Waziri wa Maliasili na Utalii, Angellah Kairuki amelitaka Shirika la Utalii Duniani – UNWTO, kuzingatia usawa katika kutoa ajira, ikiwemo masuala ya kijinsia.

Kairuki, ametoa wito huo wakati akichangia mjadala katika kikao cha kamati ya Programu na Bajeti ya UNWTO, huku Tanzania ikiwa ni mjumbe anayemaliza muda wake, kilichofanyika jijini Samarkand, Uzbekistan.

Amesema, Tanzania ipo tayari kuendelea kufanya kazi na Shirika la Utalii Duniani hasa kupitia miradi mbalimbali inayotekelezwa na Shirika hilo na pongeza juhudi zao za kuandaa Mkakati utakaounganisha Utalii na maendeleo ya kiuchumi kwa wazawa.

Aidha, Kairuki pia aliwashukuru UNWTO na UNDP kwa kutoa mafunzo ya Kutangaza Utalii kwa njia za Kidigitali, kwa Wadau wa Chama cha Wasafirishaji Watalii Tanzania – TATO.

Serikali kuweka misingi imara kuwainua Wanawake kiuchumi
Ujenzi wa Stendi usiwe chanzo Watu kwenda Gerezani - DC Sima