Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema Serikali imeazimia kuharakisha kuzindua mkakati wa kitaifa wa mawasiliano nchini, ambapo hatua hiyo inalenga kuhakikisha kuwa taarifa na ujumbe muhimu unatoka na kuwasilishwa kutokana na vyanzo vya kuaminika.

Waziri Nape ameyabainisha hayo na kusema kuwa lengo la hatua hiyo ni kukomesha habari za upotoshaji na kupiga vita habari za uongo bila kuingilia uhuru wa kujieleza.

Amesema, “mara nyingi tumejikuta tukiingia kwenye mlolongo wa kauli na ufafanuzi kutoka kwa watu wanaodai ni watoa taarifa, hasa wakati wa majanga na matatizo mengine… tunataka kukamilisha mkakati huu mwaka wa fedha ikiwa katika hatua ya juu.”

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye.

Aidha, amesema kuwa mkakati huo wa kitaifa utawawezesha Watanzania kusoma taarifa sahihi na sio suala la mikakati ya uwazi wa mawasiliano lakini kuzipata kwa wakati bali pia kuboresha upatikanaji wa habari kutoka kwa vyanzo vinavyoaminika.

Serikali imejizatiti kutatua changamoto za mawasiliano, ili kuhakikisha kuwa kuna mawasiliano ya uhakika miongoni mwa Watanzania, utoaji huduma bora za mawasiliano na nafuu kwa wananchi.

Neymar asimulia hisia za Kombe la Dunia
Dar24 yaupiga mwingi, yazoa tuzo saba EJAT