Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Costa Rica, Paulo Cesar Wanchope, ametangaza kujiuzulu nafasi yake baada ya purukushani zilizojitokeza siku ya jumanne wakati wa mchezo wa kuwania nafasi ya kufuzu kucheza michuano ya Olympic dhidi ya Panama.

Wanchope alichukua maamuzi hayo jana, baada ya kuwa na kikao kirefu na viongozi wa shirikisho la soka nchini Costa Rica, ambao walitaka kufahamu mustakabali wake kufuatia utovu wa nidhamu aliouonyesha uwanjani.

Wanchope, ambaye aliwahi kucheza nafasi ya ushambuliaji kwenye klabu za Derby County, West Ham United na Manchester City zote za nchini England kabla ya kwenda kumalizia soka lake nchini Hispania katika klabu ya Malaga, alionekana akirushiana Makonde na askari uwanjani huko Panama city.

https://youtu.be/mF5kMS0Mom0

Wanchope alizichapa baada ya kuzozana na mlinzi aliyekuwa akizuia mmmoja wa vijana wasiingie eneo alilokuwa akilinda, lakini Wanchope akafungua na kumuingiza.

Hali hiyo ilimfanya mlinzi huyo kupandwa na hasira na kuanza kumshambulia Wanchope ambaye alijibu mashambulizi.

Hata hivyo kabla ya kuchukua maamuzi ya kujiuzulu nafasi ya kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Costa Rica, Wanchope waliomba radhi kwa tukio hilo na kusema anapaswa kusamehewa kama wanaadamu wengine waliowahi kufanya makossa na kuomba msamaha.

Katika mchezo huo wa kuwania kucheza michuano ya Olympic ya mwaka 2016, timu ya taifa ya Costa Rica ilikua ikipambana na Panama, kwenye mji wa Panama City.

Upepo Wa Usajili Wa Pedro Wabadili Muelekeo
Octopizzo Ashindana Na Dr. Dre, Ashangaa ‘Sheng’ Ilivyotusua