Utulivu umeelezewa kutawala nchini Kenya mara baada ya kumalizika kwa muda wa kupiga Kampeni nchini humo, huku uchaguzi mkuu wa nchi hiyo ukitarajiwa kufanyika Agosti 8, mwaka huu.
Kura za maoni zinaonyesha kuwepo kwa kinyanganyiro kikali kati ya Rais wa sasa wa nchi hiyo, Uhuru Kenyatta na kiongozi wa muungano wa vyama vya upinzani nchini humo (NASA) Raila Odinga, huku kukiwepo na hofu kubwa ya kutokea machafuko.
Aidha, miaka 10 iliyopita zilishuhudiwa ghasia mbaya nchini humo mara tu baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi mkuu ambapo Rais wa sasa, Uhuru Kenyatta aliibuka mshindi.
Vile vile, mafanikio makubwa katika mifumo ya kidijitali ya tume huru ya uchaguzi na mipaka itasaidia kuondoa malalamiko ya wizi wa kura, hivyo uchaguzi kuwa wa haki na huru, pia kutaepusha kutokea kwa ghasia.
Hata hivyo, Mwaka 2013 Raila Odinga alitoa malalamiko ya kuwepo udanganyifu katika matokeo ya uchaguzi huo, kitu ambacho kilipelekea kufungua kesi ya kupinga matokeo hayo.