Makazi bandia kwa Wapalestina katika eneo la Gaza na kutumikishwa kazi za ujenzi na mashamba imepelekea kukua kwa kiwango cha ujasusi katika kikundi cha wapiganaji cha Hamas, kilichosababisha mashambulizi yaliyopelekea machafuko katika Taifa la Israel.
Akizungumza na Dar24 Media Mchambuzi wa Masuala ya Kisiasa, David Rwenyagira amesema baadhi ya wakazi wa Gaza hawana uwezo wa kufanya shughuli za kiuchumi, zaidi ya kutegemea misaada ambayo mdhibiti wa kupokea misaada hiyo kwa njia ya anga ni Taifa la Israel.
Amesema,“ inawezekana pia wameongeza kiwango cha ujasusi ikumbukwe pia walikuwa wanatumika kufanya kazi za mashamba na shughuli za ujenzi na kuweza kuingilia mifumo ya kiujasusi na inawezekana watu waliokuwa wanafanya hizo kazi wanauwezo wa kufanya kazi za kijasus pia wanachokitegemea kikubwa ni misaada ya kimataifa na hawawezi kuchimba mafuta wala shughuli za uvuvi.”
Aidha, Rwenyagira amesema mzozo baina ya Israel na Palestina ni historia ya tangu enzi kulingana na Imani tofauti za watu na kwamba, “ni jambo ambalo linategemea mtu amejikita sehemu gani historia yake inatokana na Imani tofauti. Pia mataifa hayo yanakinzana kiimani, ikiwemo Wayahudi, Wakristo na Waislamu kuamini kila mmoja ni eneo lake.
Hata hivyo, Israel inatarajia kuanzisha operesheni ya ardhini dhidi ya kundi la Hamas lililoshambulia kusini mwa Israel Oktoba 7. Umoja wa Ulaya,Marekani na ujerumani na hata nchi nyengine huichukulia Hamas kuwa kundi la kigaidi.