Marais wa Uturuki, Iran na Urusi wamesema kuwa wameungana ili kuhakikisha amani inapatikana nchini Syria na kuwalinda raia wa nchi ambao wamekuwa wakiteseka kwa muda mrefu.

Taarifa hiyo ya pamoja ya viongozi hao, Recep Tayyip Erdogan, Vladimir Putin na Hassan Rouhani iliwekwa katika  tovuti ya rais wa Iran baada ya kumalizika kwa mkutano huo uliofanyika mjini Ankara nchini  Uturuki.

Aidha, Viongozi hao walifanya mkutano na kila mmoja wao kwa nyakati tofauti kabla ya kuanza kwa mkutano wa  pamoja ambao uliiweka kando Marekani ambayo ina vikosi vya majeshi nchini Syria.

Hata hivyo, Rais wa Iran, Hassan Rouhani ameitupia lawama Marekani kwa kuliunga mkono kundi la wanamgambo  linalojiita Dola la Kiislamu nchini Syria na kutoa wito kwa nchi zote kuheshimu uhuru wa mshirika wake mkubwa  katika mataifa ya kiarabu katika mashariki ya kati.

 

Liverpool yaipoteza maboya Manchester City
Video: Mbowe atoa msimamo mkali, Vyama vinavyovunja sheria sasa kufutwa