Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan amesema kuwa anatarajia kupokea mfumo wa ulinzi wa makombora wa S-400 kutoka Urusi kuanza kuwasili nchini humo mwezi Julai.
Taarifa hiyo imeripotiwa na shirika la habari la NTV, hali ambayo inatarajiwa kuibua mvutano mkali kati yake na jumuiya ya kujihami ya NATO ambayo Marekani ni mwanachama.
Akiwa katika ndege baada ya ziara yake huko Tajikistan, ambapo alihudhuria kongamano na kukutana na rais wa Urusi, Vladimir Putin, rais Erdogan amesema kuwa walijadiliana kuhusu suala hilo la mfumo wa S-400 na Urusi na kwamba limekamilika.
Aidha, kaimu waziri wa ulinzi wa Marekani, Patric Shanahan mwezi huu alitoa onyo kwa Uturuki kwa vile itakavyoondolewa katika mpango wa ndege za kivita za F-35 iwapo haitabadili mpango wake wa kununua mfumo huo wa makombora.
-
Uturuki kupokea mfumo wa kujilinda na makombora
-
Mke wa waziri mkuu atozwa faini
-
Mabalozi wa Marekani waunga mkono mapenzi ya jinsia moja
Hata hivyo, rais Erdogan amesema kuwa atajadili suala hilo na rais wa Marekani, Donald Trump watakapokutana katika kongamano la mwezi huu la mataifa yenye nguvu duniani G20.