Jeshi la Uturuki limetangaza kuwakamata makomando wanaotuhumiwa kufanya njama za kumteka Rais wa nchi hiyo, Recep Tayyip Erdogan kufuatia jaribio la mapinduzi lililoshindikana mwezi uliopita.

Rais Recep Tayyip Erdogan

Rais Recep Tayyip Erdogan

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Jeshi hilo, kikosi maalum kilifanikiwa kuwatia mbaroni makomando 11 karibu na Marmaris kwa kutumia ndege zisizokuwa na marubani zilizobaini eneo walilopo.

Imeelezwa kuwa makomando hao walijipanga msituni kwa muda kufanikisha tukio hilo wakati Rais huyo alipokuwa mapumzikoni Kusini Magharibi mwa Uturuki, usiku ambao kulifanyika jaribio la mapinduzi.

Tangu kufanyika kwa jaribio hilo la Mapinduzi, makumi elfu ya wanajeshi wanaotuhumiwa wametiwa mbaroni ikiwa ni pamoja na baadhi ya majaji na watumishi wa umma wanaohusushwa na mpango huo.

Mrema alia na Paul Makonda kuhusu Bodaboda
Wakulima, Wafugaji na Wavuvi wataongeza Ari ya Uzalishaji Viwandani - Majaliwa