Serikali ya Uturuki imefanikiwa kununua mfumo wa silaha ambao ni tishio kwa Serikali ya Marekani licha ya kupata pingamizi kali kutoka nchi hiyo.
Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan amesema kuwa ana matumaini kwamba mfumo wa kujilinda dhidi ya makombora ya urusi ambao Washington unauona kama ni tishio kwa ndege za Marekani utawasilishwa nchini humo mwezi julai.
Marekani imeendelea kuwaonya Uturuki kuwa haiwezi kuwa na mfumo huo wa S-400 pamoja na ndege za kivita za Marekani aina ya F-35 huku Rais Erdogan wa Uturuki akiendelea na msimamo wake kuwa watamwajibisha mtu yeyote atakaye iondoa katika mpango huo.
Uturuki huzalisha vipande 937 vya ndege za F-35, tayari imetia saini ya kununua ndege 100 aina ya F-35 na imewekeza vya kutosha katika mpango huo wa silaha za F-35
Licha ya mvutano uliopo baina ya Uturuki na Marekani juu ya umiliki wa silaha hiyo, Rais, Edogan amesema kuwa anatumai kutatua mvutano wao kwa njia za kidiplomasia kabla ya mkutano na rais Trump mwisho wa mwezi juni.
Nchi ya Uturuki ambayo ni mwanachama wa NATO imekuwa ikipigania sera ya ulinzi kwa uhuru na imeimarisha uhusiano wake na Urusi kufuatia kuharibika kwa uhusiano wake na Marekani pamoja na mataifa ya Ulaya.
Uturuki ina jeshi la pili kwa ukubwa katika NATO, muungano wa kijeshi wa mataifa 29 ulioanzishwa kujilinda dhidi ya muungano wa Soveiti.
Mfumo wa S-400 ni moja ya silaha ya hali ya juu duniani inayotoa ulinzi wa ardhini na angani, ina uwezo wa kuangusha makombora 80 yaliyorushwa umbali wa kilomita 400 kwa wakati mmoja.
Urusi ambayo inawafundisha wanajeshi wa Uturuki kutumia silaha hiyo imesema kuwa inauwezo wa kuangusha makombora yanayorushwa kutoka kwa ndege zisizo na rubani na makombora ya masafa marefu,