Kutokana na unywaji wa pombe uliokithiri nchini Zimbabwe na kuonekana kudhoofisha utendaji wa kazi na afya za wananchi, Serikali ya nchi hiyo imependekeza muswada unaowataka wauzaji wa pombe kutouza bidhaa hiyo katika siki za wiki na wajawazito kutotumia kilevi chochote.

Serikali imesema zuio la uuzaji wa pombe katika siku ya jumatatu hadi ijumaa ni maalumu kwa lengo la kuimarisha afya za wananchi na kuongeza ufanisi wao katika kazi za uzalishaji.

Kupitia Waziri wa zamani wa afya wa Zimbabwe na Mshauri wa Wizara ya Afya na Ofisi ya Rais na Baraza la Mawaziri, Timothy Stamps ameomba pendekezo hilo kujadiliwa mapema bungeni ili sheria iweze kupitishwa mapema iwezekanavyo.

Ambapo kamati ya Baraza la Mawaziri limepitisha muswada huo wa sheria ya kupiga vita uuzaji wa pombe katika siku za wiki na kuzuia kabisa wajawazito kutumia kinywaji chenye kilevi.

Hata hivyo baadhi ya tafiti zilizofanywa zinaonesha kuwa Zimbabwe  ni nchi ya 14 barani Afrika kwa utumiaji wa pombe ambapo mtu mmoja hutumia wastani wa lita 5.1 kwa mwaka.

 

 

Rodriguez aanza Bundesliga kwa kishindo
LIVE: Rais Magufuli akihutubia wananchi Manyara