Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) umemvaa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa wakimtaka aeleze siri za chama hicho alizodai kuzifahamu.

Tamko hilo la UVCCM limetolewa leo jijini Dar es Salaam na Kaimu Katibu Mkuu UVCCM, Shaka Hamdu Shaka alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Shaka amemtaka Lowassa kujitokeza hadharani na kusema siri hizo huku akidai kuwa mwanasiasa huyo mkongwe hajui siri yoyote bali wao ndio wanaojua siri za Chadema.

“Tunamtaka Lowassa ajitokeze hadharani aeleze ni siri gani anazozijua. Na sisi tunamwambia kwamba siri ziko kwao. Na sisi vijana wa Chama Cha Mapinduzi tutaudhihirishia ulimwengu kuwa tunazijua siri za Chadema siku ya tarehe 7,” alisema Shaka.

Shaka amemtaka Lowassa kusahau kuhusu kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na badala yake apumzike kwa kile alichodai ‘hana pa kutokea’.

Majaribu: Chadema watangaza maandamano hadi 'Chato'
Mahafali Chuo Kikuu Muhimbili yasitishwa, Wanafunzi walimualika Lowassa