Hali ya kisiasa visiwani Zanzibar inaendelea kuchukua sura mpya ambapo harufu ya mpasuko ndani ya Chama Cha Mapinduzi imeanza kusikika.

Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) jana ulipendekeza chama hicho kumfuta uanachama rais mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume kwa madai kuwa anashirikiana na wapinzani kukihujumu chama hicho.

Rais Mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume

Rais Mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume

 

Kauli hiyo ya UVCCM ilitolewa jana na mwenyekiti wa Umoja huo Taifa, Sadifa Juma Khamisi katika kilele cha matembezi ya kumbukumbu ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Sadifa alieleza kuwa endapo CCM haitachukua hatua ya kumfukuza, umoja huo utatumia utaratibu tofauti kumuondoa.

Hata hivyo, leo Karume alihudhuria sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar na pale jina lake lilipotajwa na rais Ali Shein, umati uliofurika ulimshangilia kwa nguvu kubwa. Viongozi wa kitaifa wa Chama cha Wananchi (CUF) akiwemo makamu wa kwanza wa rais, Maalim Seif Sharif Hamad hawakuhudhuria sherehe hizo.

Louis Van Gaal Achoshwa na Manchester United
Ronaldo akiri kuutamani mguu wa Messi