Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umesema kuwa uamuzi wa kumpokea Waziri Mkuu Mstaafu na aliyekuwa Mgombea Urais kupitia Chadema, Edward Lowassa, umefuata taratibu sawa na wanachama wengine lakini pia umetoa somo kwa vijana kufahamu hakuna mkamilifu kwenye safari ya kisiasa.
Hayo yamesemwa jijini Dodoma na Mwenyekiti wa UVCCM, Kheri James, ambapo amesema kama Lowassa angepokelewa kinyume na chama hicho, umoja huo ungesimama kukemea.
“Tunawapongeza viongozi wakuu wa Chama kwa kitendo cha kumpokea Lowassa. amerudi CCM kwa kuzingatia taratibu zote kama wanachama wengine. Lowassa ni raia wa Tanzania kuhamia Chadema hakumuondolei haki ya kurejea CCM,” amesema James
Amesema kuwa milango ipo wazi kwa wanasiasa wengine wenye kutaka kuhamia CCM kwani mtaji wa chama chochote cha siasa ni wanachama.
Aidha, Mwenyekiti huyo ambaye aliambatana na viongozi waandamizi wa UVCCM, amesema viongozi wa kisiasa wanapaswa kuwa watiifu kwa sheria za nchi.
Hata hivyo ametangaza mchakato wa kuziba nafasi ya aliyekuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) upande wa vijana, Sophia Kizigo ambaye aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma.
-
Video: Lowassa msiniulize kwanini nimerudi, atoa agizo kwa wapiga kura wake
-
Lowassa anena awaomba waliompa kura mil.6 warudi CCM
-
Polepole ‘alivyomfagilia’ Lowassa