Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi CCM, (UVCCM), umewataka watendaji wake kufuata taratibu na sheria za chama hicho na kuongeza kuwa atakayeenda kinyume na kanuni na maadili ya Jumuiya hiyo atachukuliwa hatua kali.
Hayo yamesemwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka alipokuwa akizungumza na watendaji wa jumuiya mkoa wa Katavi na Rukwa.
Amesema kuwa Jumuiya hiyo inataarifa za kutosha kuhusu watendaji hao kutumiwa na maadui wa chama hicho ili kutaka kudhoofisha mikakati ya umoja huo.
“Kuna mikakati batili inayoratibiwa na baadhi ya watendaji ambao naimani hawatafanikiwa kwakuwa tayari taarifa zao tumeshazipata na naamini hawatafanikiwa kuichafua jumuiya
yetu kwa vyovyote vile,”amesema Shaka.
Hata hivyo, Kaimu Katibu Mkuu huyo wa UVCCM amehitimisha ziara yake ya kuimarisha chama na Jumuiya zake katikaKmikoa ya Katavi na Rukwa huku akitarajiwa kuanza ziara katika mkoa ya Pwani na Dar es salaam