Umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi, UVCCM umeitaka jeshi la polisi kuhakikisha inakomesha matumizi ya vikundi vya ulinzi hususani kikosi cha Red Brigade kinachotumiwa na Ukawa.

Tamko la UVCCM limetolewa jana na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu alipokuwa anaongea na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam ambapo amedai kuwa umoja huo uko tayari kwa lolote endapo Ukawa watatumia vijana wao kushambulia CCM.

“Tuko tayari kwa lolote wanavyotaka na kama mbwai iwe mbwai, hatuko tayari kuona amani ya nchi hii inachezewa kwa kisingizio cha demokrasia, uendeshaji wa vyama vya siasa usichukuliwe kama mwanya wa udhaifu,” alisema.

Alisisitiza kuwa jeshi la polisi linajukumu la kuchukua hatua na kupiga marufuku matumizi ya vikundi hivyo.

Green Guard ya CCM

Green Guard ya CCM

Msajili wa vyama vya siasa nchini, Jiji Francis Mutungi aliwahi kupiga marufuku matumizi ya vikundi vya ulinzi vya vyama vya siasa. Wakati Ukawa wameanza matumizi ya Red Brigade, CCM hutumia Green Guard.

 

Esther Bulaya Aigawa Chadema Bunda
Lowassa Kimyaaa… Anasubiri Mlio Wa Kipenga