Klabu ya Stoke City itamsajili mshambuliaji kutoka nchini Uswiz na klabu ya Inter Milan ya Italia, Xherdan Shaqiri, baada ya ofa yao ya Euro million 17 ambazo ni sawa na paundi milioni 12 kukubaliwa huko mjini Milan.

Shaqiri, ataondoka mjini Milan baada ya kusajiliwa na Inter Milan mwezi Januari mwaka huu akitokea kwa mabingwa wa soka nchini Ujerumani FC Bayern Munich na ameonekana kushindwa kumridhisha meneja wa The Nerazzurri Roberto Mancini.

Stoke City waliwasilisha ofa yao jana jioni kwa sharti la kulipa kiasi cha paund million 15 kwanza na baada ya miezi sita watamalizia paund million 2 katika usajili wa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23.

Mourinho: Sikupingana Na Roman Abramovich kuhusu Petr Cech
Van Parsie Kuwa Mbadala Wa Demba Ba, Ligi Ya Uturuki