FC Barcelona jana Septemba 24 walisheherekea miaka 63 ya umri wa uwanja wao wa Camp Nou, ambao umekua na mvuto wa aina yake katika michezo ya ligi ya Hispania na ile ya kimataifa.

Uwanja huo mkubwa wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 99,354, ulizinduliwa rasmi mwaka 1957, kwa mara ya kwanza uliitwa Camp de Corts.

Baadae jina hilo lilibadilishwa na kuwa Estadio Del CF Barcelona, huku jina la Camp Nou/Nou Camp likianza kutumika mwaka 1975.

Uwanja wa Nou Camp ndio uwanja mkubwa kuliko yote barani Ulaya ngazi ya klabu. Ubora wa uwanja huu katika sehemu ya kuchezea wachezaji ni jambo la kuvutia sana.

Baadhi ya wachezaji wanavutiwa sana kucheza Nou Camp na wengine huwa vigumu kuweza kuhimili makelele ya mashabiki yanayotoka kila upande wa jukwaa.

Uwanja huu umewahi kuwa mwenyeji wa fainali mbili za Ligi ya Mabingwa barani Ulaya. Ulitumika pia katika hatua ya nusu fainali ya Kombe la Dunia zilizofanyika nchini Hispania mwaka 1982.

Vile vile uwanja huu ulipata kuwa mwenyeji wa mashindano ya Olimpiki mwaka 1992. Wabunifu wa uwanja huu ni Francess Mutjans na Josep Soteras.

Kumbuka ukiwa Camp Nou siti yako hawezi kukaa mtu mwingine. Hapo hapo kumbuka kwamba ukiingia ndani na hauelewi lolote kuhusu siti yako iliyopo kuna kina dada warembo saaana walio tayari kukupeleka mpaka siti yako ilipo.

Bah N'Daw kuapishwa kuwa rais wa mpito nchini Mali
Panya buku wa Tanzania apata nishani ya dhahabu Uingereza

Comments

comments