Uongozi wa klabu ya Dodoma jiji FC umethibitisha taarifa za kuruhusiwa kutumia uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, baada ya kufanyiwa ukaguzi na Bodi ya Ligi Kuu.

Uwanja wa Jamhuri ulifungiwa kutumika kwa michezo ya Ligi Kuu kwa kukosa vigezo kwa mujibu wa kanuni mwishoni mwa mwezi uliopita, hatua ambayo ilipelekea timu ya Dodoma Jiji FC kutumia kwa muda uwanja wa Samora mjini Iringa.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa mchezo ujao wa Ligi Kuu dhidi ya Biahsra United Mara utachezwa uwanja wa Jamhuri, hivyo mashabiki wa Dodoma jiji wameombwa kufika uwanjani hapo kuishangilia timu yao.

Hata hivyo Bodi ya Ligi nayo imethibitisha kuufunguliwa uwanja huo, baada ya kuridhishwa na maboresho yaliyofanywa uwanjani hapo.

Dodoma jiji inarejea katika michezo ya Ligi Kuu, baada ya kupisha kalenda ya FIFA.

Watu 7 wauawa katika maandamano Uganda
Mwinyi awaachia ACT-Wazalendo Wizara mbili

Comments

comments